<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>37</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Waitwa, mwovu, na Bwana
 Umwendee hima sana,
 Usafiwe dhambi zako,
 Humwoni ni mwema kwako?

[V2]
 Unaitwa! Itika tu!
 Umwendee Bwana Yesu!
 Sifiche makosa yako,
 Uungame dhambi zako!
 Kristo tu umuamini,
 Ndiye njia ya Mbinguni.

[V3]
 Alilipa damu yake
 Ili kukukweza kwake;
 Alikufa yeye Bwana,
 Mimi nawe tuwe wema.

[V4]
 Ukifanywa kuwa mwema
 Mwishoni utasimama,
 Utaingia rahani
 Na wapenzi wa zamani.

[V5]
 Ni mwanga tu, nchi ile;
 Uovu hauko kule,
 Kwamba wataka ufike
 Sharti huku uosheke.</lyrics>
<title>Waitwa, Mwovu, Na Bwana TZR37</title>
</song>